Hayo yamesemwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo na Hakimu Flora Lymo anayesikiliza kesi hiyo.
Wakati wa kesi hiyo, mtuhumiwa Scorpion aliomba asomewe maelezo ya awali lakini hakimu Lymo alikataa.
Scorpion anadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo anatuhumiwa kuiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ukiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.
Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo iliyovuta hisia nyingi za watu hususani wakazi wa jijini Dar ulinzi ulikuwa mkali muda wote.
