Kesi ya kupinga uchaguzi wa Umeya na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni iliyofunguliwa na Chadema katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepangwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage na imepewa namba 304 ya 2016.
Katika kesi hiyo Chadema kupitia wakili wake, John Malya wanaiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itengue uchaguzi huo.
Pia wanaomba mahakama iamuru uchaguzi huo uitishwe upya na walipe gharama za kesi.
Walalamikaji katika kesi hiyo ni Mustafa Abdul Muro na Jumanne Mbunju dhidi ya Benjamin Sitta, Manyama Mangaru, Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Kinondoni, Msimamizi wa mkutano huo na Meya na Naibu Meya wa Kinondoni.
Mwanasheria wa chama hicho, John Malya alisema wamefika mahakamani hapo ili kueleza walichokifanya si sahihi na kwamba wamekwenda mahakamani hapo kwa ajili ya kutafuta haki.