Jamaa ajichinja baada ya mpenzi wake kuchukuliwa na mwanaume mwingine


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamme mmoja ambaye hajajulikana jina anayedaiwa kuwa ni mfanya biashara katika stendi ya mabasi ya Mpwapwa mkoani Dodoma amejichinja kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog limetokea leo Oktoba 25,2016 majira ya saa sita mchana baada ya jamaa huyo kukataliwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.

“Amejikata koromeo kwa kutumia kisu baada ya mwanamke aliyekuwa naye kumkataa kwa madai kuwa ana mwanamme mwingine,kitendo cha mpenzi wake kuchukuliwa na mwanamme mwingine ndicho kimemfanya achukue maamuzi hayo magumu ya kuondoa uhai wake”,mashuhuda wameiambia Malunde1 blog.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo pamoja na mwanamme anayedaiwa kuchukua mpenzi wa mwanamme aliyejichinja pia wanafanya kazi katika stand hiyo ya mabasi.

Hata hivyo kutokana na kitendo hicho wasamaria walijitokeza kumsaidia mwanamme huyo na kumkimbiza katika hospitali ya wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya matibabu.

Chanzo: Malunde blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo