Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ikiwa Kazini Barabara ya Ikonda Hospitali





Halmashauri ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe imeendelea na ufumbuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake hasa kuimarisha barabara zilizoko chini yake kabla msimu wa mvua haujaanza

Hivi sasa halmashauri hiyo imeanza ukarabati wa barabara ya kuelekea hospitali ya Consolata Ikonda kwa kuiwekea kifusi kizuri na imara ili barabara hiyo yenye matumizi makubwa kutokana na hospitali hiyo iendelee kupitika misimu yote ya Mwaka

Mwandishi wetu hii leo amepita katika barabara hiyo na kushuhudia malori yakimwaga kifusi hatua inayoashiria ni mwanzo mzuri wa Matengenezo hayo

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi alitangaza hadharani katika mkutano na wananchi wa kata ya Tandala kuwa wakati wa ujenzi wa barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha lami utakapofanyika barabara hiyo ya kuelekea hospitali ya Ikonda nayo itajengwa kwa lami na serikali ya awamu ya 5


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo