Uharibifu Mkubwa wa Mazingira katika Vyanzo Vya maji. Pichani ni kilimo cha miwa katika mto katika kijiji cha Limba, Sumbawanga. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameagiza watu hao kuondelewa mara moja.
Wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga wamevamia chanzo cha maji cha Mto Lwiche, na kujihusisha na shughuli za kilimo pamoja na upandaji wa miti ya mikaratusi inayonyonya maji, chanzo hicho ni miongoni mwa Vyanza vya maji vilivyopo hatarini kutoweka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiagiza watu kuondolewa kwa wavamizi wa vyanzo vya maji.