ZITTO Kabwe Afunguka Kuhusu Utafiti wa Twaweza Kuhusu Wananchi na Rais Magufuli

Kura za Maoni zilizotolewa na TWAWEZA zinaibua maneno ambayo unashangaa kuyasikia kwa wasomi, wengine maprofesa. Kwangu mimi naona masuala 2 muhimu

Matokeo yanaonyesha IMANI kubwa ambayo wananchi wanayo kwa Rais Magufuli. Hata hivyo IMANI hiyo inakuja na wajibu mkubwa sana na Rais asitumie vibaya imani hiyo. Kiongozi mwenye busara hawezi kutumia imani hii kwa kukandamiza demokrasia na kukanyaga Katiba.
Matokeo pia yanaonyesha kuwa Wabunge na Madiwani kwa kiasi kikubwa wana IMANI ya wananchi wao wanaowawakilisha. Huu ni wajibu na fursa kwa Wabunge wa Upinzani kuonyesha uongozi mahiri wenye kutoa majawabu ya changamoto za wananchi kwenye maeneo yanayoongozwa na Vyama vya Upinzani.

Tujifunze kukubali tusiyopenda kuyasikia. Wakati tunapambana vita adhimu sana dhidi ya Udikteta Mamboleo unaonyemelea nchi yetu, pia kwa nguvu hizo hizo tuonyeshe tofauti ya kiuongozi katika Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji tunayoongoza

By Zitto Kabwe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo