Update: Watanzania Wenzetu Waliokuwa Wametekwa huko DRC Congo Wameokolewa

Madereva wa malori kutoka Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatimaye wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo amezungumza na shirika la utangazaji la BBC na kusema wote wameokolewa   na wako salama

Taarifa iliyotolewa jana  na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilieleza kuwa watekaji hao ni kikundi cha waasi cha MaiMai ambao baada ya kuyateka magari 8 toka Tanzania , waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Bw. Dewji. 

Waasi hao walioa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo