Kundi la wakazi wa kijiji cha Nguruma kata ya Nkwarua wilaya ya Arumeru wameandamana kuvamia shamba la mwekezaji wa Arusha Coffe Estate na kung'oa alama za mipaka na kutaka kulichoma moto kwa madai kuwa mwekezaji alichukua ardhi ya wananchi zaidi ya miaka ishirini iliyopita ameshindwa kuliendeleza huku akiuza sehemu ya ardhi hiyo na kuwaacha wananchi wakiteseka kwa kukosa ardhi ya kilimo makazi na maeneo ya huduma za jamii.
kwenye shamba hilo mwandishi ameshuhudia idadi kubwa ya wananchi wakiwa wanang'oa alama za mipaka hali iliyo walazimu viongozi wa kamati ya maridhiano katika mgogoro huo kutumia nguvu kuwazuia wasichukue sheria mkononi huku wananchi wakidai kuwa ardhi hiyo ilikuwa ni ya wananchi walinyang’anywa bila fidia mwekezaji ameshindwa kuiendeleza na ameanza kuuza kwa matajiri.
Kwa upande wao wanawake kutoka katika kijiji hicho wameeleza wanavyo teseka wanapo ingia kwenye eneo hilo kutafuta kuni pamoja nanyasi za kulisha mifugo.
Akizungumza baada ya kutuliza hasira za wananchi mwenyekiti wa kamati ya mgogoro wa shamba hilo Eliud Kaaya amsema hati miliki ya shamba hilo imefutwa miaka mingi iliyo pita na waziri wa ardhi alidhibitisha hilo hivyo wanamwomba waziri awasaidie kupata haki yao.
Mwandishi wa habari hii ameutafuta uongozi wa wilaya ya Arumeru na mwekezaji anaye lalamikiwa kupata ufafanuzi wa mgogoro huo bila mafanikio lakini juhudi za kuwatafuta zanaendeleo.
chanzo: ITV