Maajabu: Kilimo cha Umwagiliaji Bangi kwa kutumia Pampu chagundulika Rukwa

Jeshi la polisi mkoani Rukwa linawashikilia wakulima wanane wa kijiji cha Fyengelezya katika manispaa ya Sumbawanga, ambao wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha umwagiliaji cha mashamba ya zao haramu la bangi, wakitumia pampu za kuvuta maji kwenye mabonde yenye mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekari kumi.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa kamishna msaidizi wa polisi George Kyando, akishiriki kikamilifu katika uvunaji na uteketezaji wa bangi hiyo, amesema tangu kukamilishwa na utengenezaji unaoendelea wa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami, mkoa huo uliokuwa hauna sifa ya kilimo hicho cha zao hilo haramu la bangi, sasa unaibuka kwa kasi jambo ambalo linapaswa kudhibitiwa kikamilifu.

Aidha kamanda huyo wa polisi amesema operesheni hiyo ni kutuma salamu, kwa wote wanaojihusisha na kilimo hicho cha zao la bangi, kwamba zoezi hilo ni endelevu na watasakwa kila eneo, huku mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho cha Fyengelezya Bw Deodatus Ramadhani, akiwataka wananchi wake wajikite kwenye kilimo cha Mahindi, Maharage na alizeti na kuachana kabisa na kilimo hicho cha bangi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo