Walimu wanne na wanafunzi nane wa sekondari ya Ole Sokoine iliyoko
wilayani Monduli mkoani Arusha wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kuhusika na matukio ya moto katika mabweni ya wanafunzi wilayani Monduli
mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Monduli Bw.Iddi Hassan amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wanahusika kwa kushirikiana na watu wengine ambao wanaendea kutafutwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Bw.Isack Joseph amesema katika kukabiliana na matukio hayo wameanza utaratibu wa kufunga vifaa vya kutoa taarifa ya moto katika mabweni yote ya wilaya hiyo.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw.Stephen Anderson amesema majanga ya moto yaliyotokea licha ya kusababisha hasara kubwa yamelewaathiri kisaikoloji walimu,wazazi na wanafunzi.
Hadi sasa mabweni ya shule tatu za wilaya ya Monduli na moja la wilaya ya Longido na moja la wilaya ya Arumeru yamechomwa moto katika matukio yanayofanana yaliyotokea kwa mfululizo katika kipindi cha wiki mbili.