Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda jana alijitokeza
katika mkutano wa Rais Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha
Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo
anatatua kero za wananchi.
Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza Rais Dkt. Magufuli , Shibuda alivitaka vyama vingine vya siasa nchini kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya watanzania wote.
"Mheshimiwa
Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi
kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa
mlenda unamwangusha mtu mzima" - Alisema Shibuda.
Shibuda alisema
vyama vya UKAWA vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni mtu
mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya
Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa taifa .
Aidha Shibuda alimuomba Rais Magufuli kwamba akipata muda aende akamweleze vizuri matatizo yanayowakabili wakulima nchini.