Rais Magufuli Ampatia Bajaji Mlemavu Anayejituma

Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi.

Bw. Thomas Kone akipanda kwenye bajaji aliyokabidhiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akisalimiana na Bw. Thomas Kone alipokwenda Kumkabidhi Bajaji kwa Niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo