PICHA: Rais Magufuli Akiweka Jiwe La Msingi Daraja Wa Waenda Kwa Miguu La Furahisha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha kuwa ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Makongoro jijini Mwanza unakamilika ifikapo disemba mwaka huu.

Aidha amesema upanuzi wa barabara ya Makongoro uliokuwa ujengwe kati ya Furahisha hadi Pasiansi Km 2.8 sasa utaendelezwa hadi kufikia uwanja wa ndege.

Akizungumza jana  mara baada ya kuweka jiwe la msingi la daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa barabara ya Makongoro Mh. Dkt. Magufuli alisema kasi ya ujenzi wa barabara jijini Mwanza uendane na ujenzi wa uwanja wa ndege ili kuwezesha mkoa wa Mwanza kuwa kitovu cha nchi za maziwa makuu.

“Nakuagiza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  uhakikishe kuwa barabara na daraja la watembea kwa miguu Furahisha vinakamilika mwezi desemba na mkandarasi wa uwanja wa ndege anaanza kazi mara moja”.
Alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.

Alisema nia ya Serikali yake ni kununua meli mbili na kujenga daraja kati ya Kigongo na Busisi ili kuboresha huduma za usafiri katika Ziwa Victoria.

Naye Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale alimtaka mkandarasi anaejenga daraja la waenda kwa miguu na barabara ya Makongoro kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Zaidi ya shilingi bilioni 6.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaopunguza msongamano wa magari na ajali katika barabara ya makongoro jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo