"Mchezo wa bao marufuku muda wa kazi"

 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amepiga marufuku wananchi wa wilaya yake kucheza mchezo wa bao na ‘pool table’ wakati wa mchana ambao ni muda wa kufanya kazi na kutekeleza falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Gondwe ameyasema hayo alipofanya mazungumzo maalumu na kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na East Africa Radio ambapo amesema baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli na kuanza kazi kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo alikuta muamko wa vijana katika kufanya kazi ni mdogo huku wengi wakishinda vijiweni kwa kucheza 'pool table' na bao jambo ambalo amepiga marufuku wakati wa kazi.

“Nimekataza vijana kucheza michezo hiyo wakati wa kazi na nimewahamasisha kushiriki shughuli za ufugaji na kilimo ambapo wilaya ya Handeni inakubali sana kilimo cha matunda, alizeti, ufuta na ufugaji wa mbuzi na kuku ambapo kwa kushirikiana na idara ya ardhi tumekubaliana kutenga maeneo ya uwekezaji kwa vijana ambapo serikali itawawezesha kuweza kuyafanyia kazi za kilimo’’ Amesema Gondwe.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewataka vijana kujiunga katika makundi ili waweze kupata fedha ambazo kila halmashauri imetakiwa kutenga asilimia 5% ya mapato yake kwa ajili ya vijana na 5% kwa ajili ya wanawake ili waweze kutumia mikopo watakayopata kujikwamua kuimaisha kwa kufanya shughuli mbalimbali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo