Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameondoka nchini
kuelekea Philadelphia nchini Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa chama
cha Democrats utakaomthibitisha Bi. Hillary Clinton kuwa mgombea urais
kupitia chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya ACT Wazalendo wakati akiwa kwenye
mkutano huo ndugu zitto atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi
mbalimbali wa kisiasa duniani.
Shughuli nyingine atakayofanya ni pamoja na kufanya kikao cha maandalizi juu ya ufunguzi wa tawi la wanachama wa ACT Diaspora la nchini Marekani pamoja na kuwa na mazungumzo maalumu na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad juu ya hali ya kisiasa ya zanzibar na taifa kwa ujumla.