Wananchi Wamkataa mwenyekiti wa kijiji

Wanakijiji wa Kijiji cha Ilasilo kata ya Galula wilaya ya Songwe Mkoani Songwe wamekataa kurudishwa madarakani kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, JUMA FULGENZI, kutokana na tuhuma za kutumia vibaya fedha za wananchi wa Kijiji hicho.

Mwenyekiti huyo alisimamishwa mwezi Aprili mwaka huu wakimtuhumu kutumia vibaya shilingi milioni 1.1 za kijiji hicho zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mwalimu Mkuu.

Wananchi hao walikataa Fulgence kurudi madarakani mbele ya Katibu Tarafa ya Songwe, GODWIN KAUNDE, alipowataka wananchi hao kumrudisha madarakani ambapo wamesema kuwa hawawezi kukubali mpaka atakapokamilisha jengo hilo kwa gharama zake mwenyewe.

Naye Mwenyekiti anayetuhumiwa kuiba fedha hizo ameahidi kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo ndani ya muda wa wiki mbili huku katibu tarafa ya Songwe GODWIN KAUNDE akiwasihi wananchi kumpa nafasi nyingine mwenyekiti huyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo