Mwenyekiti wa kijiji cha ujuni Bw. Happyniko Michael Sanga amekiri kuwepo kwa tukio la kuuawa mtoto katika kijiji chake na kusema kwamba baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji za tukio hilo, walilazimika kumbana binti Vumilia ambaye toka awali hawakuridhishwa sana na majibu yake kuwa amempeleka kwa bibi yake, na ndipo walipombana na kukiri kuwa ameuawa na kuwapeleka hadi eneo la tukio ulipokutwa mwili huo
Amesema Hali hiyo iliwalazimu kutoa taarifa kituo cha polisi Makete ambapo jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umeharibika vibaya baada ya kukaa kwenye maji kwa muda wa wiki 3, na baada ya kuchukua taarifa zao walishauriana kwa pamoja na uongozi wa kijiji na kata kuuzika mwili wa marehemu jirani na eneo la tukio kutokana na uharibifu wa mwili huo
Amesema baada ya kuuzika mwili wa marehemu polisi walifika kijijini hapo kufanya mahojiano na baadhi ya watu wakiwemo viongozi na pia kumchukua mtuhumiwa ambaye ni mama mzazi wa marehemu kumpeleka kituo cha polisi Makete kwa hatua zaidi za kisheria
Taarifa za tukio hilo zimetolewa na watoto waliokuwa wakichunga ng'ombe jirani na mto huo ambapo wakati wakienda kuwanywesha maji ng'ombe hao mtoni majira ya jioni kabla ya kuwarudisha nyumbani ndipo walipuona mwili wa marehemu na kupeleka taarifa za tukio hilo kijijini hapo
kujua zaidi ingia hapa