TCRA watembelea 91.5 Green FM, Angalia Picha zote na Sauti

Imeelezwa kuwa zoezi la uzimaji simu feki litakalofanywa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Juni 16 mwaka huu, si la kumkoamoa mtumiaji wa simu hiyo na badala yake linamnusuru na madhara mengi ambayo angeyapata

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu Kusini Mhandisi Lilian Mwangoka wakati akizungumza moja kwa moja katika kipindi maalum Kilichorushwa na 91.5 Green FM kuhusu zoezi la uzimaji wa simu feki

Mhandisi Mwangoka amesema zoezi hilo linalenga kuziacha simu halisi sokoni na katika matumizi ya kila siku, kwa kuwa simu feki zimekuwa zikitumika katika matukio mengi ya kihalifu na haziwezi kupatikana katika mitambo ya serikali, na pia zimekuwa na madhara kwa watumiaji Ikiwemo mionzi kwa kuwa hazijathibitishwa na shirika la viwango hapa nchini TBS

Pia amewasihi wananchi kutunza simu zao na kutoziacha zitumiwe na watu wengine

Awali katika kipindi hicho Mhandisi Mwangoka amepata nafasi ya kuulizwa na kujibu maswali kutoka kwa wasikilizaji waliotaka kufahamu mambo mbalimbali kuhusu uzimaji wa simu feki
  Meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu Kusini Mhandisi Lilian Mwangoka wakati akizungumza moja kwa moja katika kipindi maalum Kilichorushwa na 91.5 Green FM kuhusu zoezi la uzimaji wa simu feki

 Mtangazaji wa 91.5 Green FM Fadhili Lunati akiendesha kipindi hicho
 Jengo zilipo studio za 91.5 Green FM
 Mtangazaji wa Kipindi hicho Fadhili Lunati kutoka 91.5 Green FM akisoma meseji za wasikilizaji
Sikiliza sauti hizi hapa chini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo