Tandala wakumbuka shuka kukiwa kumekucha...Ni ishu ya Madawati

Upungufu wa madawati 40 katika shule ya msingi  Tandala Mazoezi iliyopo katika kijiji cha Tandala kata ya Tandala wilayani Makete umepelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa  kijiji cha Tandala ili kujadiliana jinsi ya kumaliza tatizo hilo la madawati

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Yoanesi Chaula amesema hapo awali shule hiyo haikuwa na upungufu wa madawati lakini baada ya wataalamu wa elimu kuja na kufanya ukaguzi  katika shule hiyo na kuelekeza kuwa kila dawati inatakiwa wakae wanafunzi wawili hali hiyo imepelekea upungufu wa madawati 40 katika shule hiyo.

Aidha mwalimu mkuu huyo amewasihi wananchi wote kuwa suala la kuchangia elimu ni la wanajamii wote bila kujali  kama anamtoto  anayesoma katika shule hiyo ama la kwani kuchangia maendeleo ni suala la jamii kwa ujumla.

Wakitoa maoni yao kuhusu kuchangia mchango huo wananchi wa wameonekana kuwa na hamasa kubwa ya kuchangia mchango huo kwani hawapo tayari kuwaona wanafunzi  ambao ni taifa la kesho wakisomea  katika mazingira magumu na  kukubaliana kuchangia shilingi 2000 kwa kila mwananchi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Andowise Memba  ametolea ufafanuzi kuhusu mchango huo na kwamba wamekubaliana baada ya wiki mbili kila mwananchi awe ameshatoa mchango huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo