Tarehe
08.06.2016 majira ya saa 08:00hrs hadi saa 15:00hrs katika kisiwa cha
Maisome kambi ya uvuvi migongo kata ya Maisome tarafa Kahunda wilaya
Sengerema mkoa wa Mwanza, katika tukio la kwanza askari wakiwa doria
katika kisiwa tajwa hapo juu wakiambatana na kamati ya ulinzi na usalama
ya wilaya ya Sengerema walifanikiwa kukamata nyavu (kokolo) haramu za
kuvulia samaki 17 na timba 81 ambayo ni mitego ya kienyeji ya kutegea
samaki, vilivyotelekezwa na wavuvi wasiojulikana baada ya kupata
taarifa za kuwepo kwa askari wanaofanya doria na misako katika maeneo
yao.
Jeshi
la polisi linaendelea na misako pamoja na doria katika kisiwa hicho kwa
kuhakikisha watuhumiwa waliotelekeza nyavu hizo haramu wanakamatwa na
wengine wanaoshirikiana nao pia wanasakwa ili kukomesha uvuvi haramu
katika kisiwa hicho, hii ni baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia
wema kwamba katika kisiwa tajwa hapo juu kuna wavuvi ambao hutumia zana
haramu katika shughuli zao za uvuvi za kila siku kitendo ambacho ni
kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Aidha
tukio lingine sawa na tarehe na majiara tajwa hapo juu kwenye kisiwa
cha Kasarazi kata ya Bulyaheke tarafa ya Buchosa wilaya ya Sengerema,
askari wakiwa doria walifanikiwa kukamata nyavu haramu za kuvulia samaki
9 na timba 04 zilizotelekezwa na wavuvi wasiojulikana baada ya kupokea
taarifa ya uwepo wa askari wanaofanya doria katika kisiwa hicho. Jeshi
la polisi bado linaendelea na upelelezi pamoja na msako wa kuwasaka
wavuvi wanaojihusisha na uvuvi haramu ili waweze kufikishwa katika
vyombo vya sheria.
Baada
ya zana hizo haramu kukamatwa ziliteketezwa kwa moto mbele ya uongozi
wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya na serikali ya vijiji hivyo na
wananchi wakishuhudia, huku msako na doria katika visiwa hivyo na visiwa
vingine vya jirani bado unaendelea.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed
Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwataka waendelee kutoa ushirikiano
kwa jeshi la polisi kwani limedhamiria kukomesha uhalifu katika mkoa wa
Mwanza na kusimamia sheria na taratibu za nchi.
Katika tukio la pili
Mnamo
tarehe 08.06.Majira ya saa 13:06 katika kijiji cha Sima kata ya Sima
wilaya ya Sengerma mkoa wa Mwanza, askari wakiwa doria walifanikiwa
kumkamata Sophia Sato miaka 54 mkazi wa kijiji cha Sima akiwa na pombe
aina ya gongo lita 64 zikiwa ndani ya nyumba yake kitendo ambacho ni
kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Inadaiwa
kuwa mtuhumiwa anafanya biashara hiyo ya kuwauzia wananchi wa kijiji
hicho pombe hiyo haramu na kuifanya kazi hiyo kama chanzo chake cha
mapato kitendo ambacho ni uvunjwaji wa sheria, ndipo jeshi la polisi
lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa
pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Aidha
katika tukio lingine sawa na tarehe tajwa hapo juu majira ya saa 13:50
katika kijiji hicho cha Sima kilichopo wilaya ya Sengerema, askari
waliokuwa doria walifanikiwa kukamata mitambo miwili ya kutengeneza
pombe haramu ya gongo na mapipa mawili yaliyotelekezwa na Elizabeth
Martine aliyetoroka baada ya kupewa taarifa za uwepo wa askari
wanaofanya doria.
Inadaiwa
kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu amekuwa akijihusisha na utengenezaji wa
pombe hiyo haramu kwa muda sasa, na amekuwa akiwauzia wakazi wa kijiji
hicho. Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa
pamoja na kuwasaka wahusika wengine anaoshirikiana nao katika biashara
hiyo haramu ya pombe ya gongo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed
Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwaomba waendelee kushirikiana na
jeshi la polisi ili tujenge sote kwa pamoja Mwanza salama zaidi na
kuweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.
Imesainiwa na:
Sacp: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) mwanza