Sukari yaadimika katika baadhi ya Maeneo Makete (Audio)

Licha ya kauli iliyotolewa na Afisa biashara wilaya ya Makete Bw.Edonia Mahenge kwamba sukari imeanza kupatikana baada ya kuadimika kwa muda, imeelezwa kuwa kata ya Ipelele tarafa ya Magoma wilayani hapa bidhaa hiyo imekuwa ni adimu.

Akizungumza nasi kwa njia ya simu diwani wa kata ya Ipelele Mh. Mwipelele Mbogela amesema bidhaa ya sukari katika kata hiyo imekuwa adimu na inapopatikana huuzwa kwa shilingi 3,500/- kwa kilo moja.

Mh. Mwipelele amesema kuwa upatikanaji wa sukari kwa hivi sasa ni mgumu huku akisema kuwa serikali ilitakiwa ishughulike na bidhaa zingine ikiwemo vinywaji vikali na sio sukari kwani ni bidhaa muhimu inayohitajika katika matumizi ya kila siku ya mwanadamu.

Na Fadhili Lunati


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo