Na Francis Godwin, Iringa
Aliyekuwa mbunge wa kwanza wa Ludewa Violeth Baraka amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa mbunge wa kwanza wa Ludewa Violeth Baraka amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Taarifa kutoka kwa familia ya mbunge huyo zinadai kuwa kabla ya kifo chake mama Baraka alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na jana usiku alikutwa na mauti. mwili wake unategemewa kuzikwa kesho Ijuma jijini Dar es Salaam.
Marehemu Baraka alikuwa mbunge wa Ludewa kati ya mwaka 1965 hadi 1970. Na ndie mbunge wa kwanza kupigania Meli ya kwanza kufika katika Ziwa Nyasa meli ya MV Songea baada ya kilio cha wana Ludewa miaka hiyo. Meli iliwasili baada ya kulia na kutunga nyimbo kuwa wananchi wa Ludewa tunalilia Meli hiyo si tu kwa jimbo la Ludewa.
Mama Baraka
atakumbukwa si Ludewa pekee bali atakumbukwa kwa majimbo yote ya
mwambao mwa ziwa Nyasa.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahali pepa peponi Amen
Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahali pepa peponi Amen