Mambo matano yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Zitto Kabwe na Polisi

Leo June 08 2016 Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefika Makao makuu kanda maalum ya Dar es salaam, ikiwa ameitikia wito wa polisi. Zitto amefika kituoni hapo na ametakiwa atoe maelezo kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa June 5 2016.

Kupitia ukurasa wake wa facebook chama cha ACT Wazalendo kimeainisha masuala matano muhimu yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.

1.Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa ‘Kujenga Chama’ Lakini Chama Kilizindua “Operesheni Linda Demokrasia”.

2. Kusema “Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini” 

3. Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni “Vilaza” 

4. Kumgombanisha Rais na Wananchi kwa Kusema “Yeye anajifanya Rais wa Masikini (Huku akiwakashifu hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita “Vilaza”) na hivyo kumgombanisha na wasio Masikini” 

5. Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla 

Kupitia ukurasa huo wametoa taarifa kuwa maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa yote hayo yanaangukia kwenye Kifungu Cha 89(1)(a) cha Penal Code, Yaani “Kutumia Maneno ya Matusi yenye Kuweza Kuvunja Amani” (Abusive Language).

Jeshi la Polisi limemuomba Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi. Mwanasheria wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani Juu ya Suala Husika, Na Kwamba Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli Na Undani wa Masuala hayo Mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo