JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia, Mwananke mmoja
alietambulika kwa jina la Rosemary Khiwili (23) mkazi wa Kimara kwa
kosa la kutupa mtoto katika shimo la choo.
Rosemary
ambaye ni mfanyakazi wa Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam
anadaiwa kumtupa mtoto mchanga katika choo cha shimo cha nyumba
anayoishi na mtoto huyo amegundulika na mama mwenye nyumba, Upendo Mboma
baada ya kuingia kwa ajili ya kumwaga maji machafu na ndipo aliposikia
mtoto analia kutokea kwenye choo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa
tukio hilo lilitokea Juni 8 mwaka huu huko maeneo ya Kimara Wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kamishina,
Sirro amesema mtoto huyo aliokolewa na akiwa hai na kikosi cha Zimamoto
na uokoaji cha jiji kwa kushirikiana na askari polisi , na mtoto huyo
amehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa uangalizi maalum huku
upelelezi ukiendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa
hatua zaidi.
Wakati
huo huo jeshi la polisi limeokota silaha mbili zilizotengenezwa
kienyeji pamoja risasi sita zikiwa kwenye begi katika shamba la matuta
ya viazi baada kutelekezwa na watu wasiojulikana na jitihada
zinaendelea kuwabaini watu hao.
Kamanda,
Sirro amesema katika operesheni ambayo wanaifanya kwa wiki hii wameweza
kuwakamata watu 711 kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu,
kukutwa bhangi na Gongo , mitambo ya kutengeneza gongo, kucheza kamari
pamoja na biashara ya kuuza mwili.
Amesema Kawe pamoja na Mabibo zinaongoza kwa utengenezaji na uuzaji wa pombe haramu ya Gongo.