Damu yamwagika huko Morogoro...27 Wajeruhiwa

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 35 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya NBS lenye namba za usajili T 909 BXK lililo kuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Tabora kuanguka katika eneo la Tabu Hotel kata ya Chigela wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Mganga wa hospitali ya wilaya ya Gairo Mushi Mabula amethibitisha kupokea maiti tano na majeruhi 26 ambapo amesema watu saba hali zao sinzuri na watahamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
 
Kwa upande wao mashuhuda wakiwemo majeruhi wa ajali hiyo wameeleza jinsi ajali hiyo ilivyotokea huku mashuhuda wakiwataka madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
 
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakilazwa katika hospitali ya wilaya ya Gairo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo