Mtoto wa mwaka mmoja agundulika kuwa na nguvu za kiume na hamu ya ngono

Mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja nchini India aliyebainika kuwa na nywele kwenye sehemu zake za siri na hamu ya kufanya mapenzi amegundulika kuwa na tatizo la homoni ambalo ni nadra sana.
Mtoto huyo ambaye jina lake ni Akash, alipatikana akiwa na homoni za testosterone zenye kiwango cha mtu mzima mwenye miaka 25. Hiyo inamaanisha kuwa alikuwa na uume wenye size kama ya mtu mzima, ndevu na nywele za sehemu za siri pamoja na sauti isiyoendana na umri wake.

Madaktari sasa wanadai kuwa mtoto huyo ana tatizo liitwalo precocious puberty ambapo mtoto hubalehe kabla ya miaka saba au nane.

Wazazi wa Akash mwanzoni waligundua kuwa kuna kitu hakipo sawa kwa mtoto wao alipokuwa na miezi sita. Uume wake ulikuwa ukiwa mkubwa kuliko kawaida, wakati mwili wake ulikuwa mdogo mno ukilinganisha na watoto wa umri wake.

“Tulidhani labda alikuwa mtoto mkubwa, hivyo hatukumpeleka kwa daktari,” mama wa mtoto huyo aliliambia gazeti la Hindustan Times.

“Lakini alipofikisha mwaka mmoja, ilikuwa wazi kuwa kuna kitu hakikuwa sawa. Mama mkwe wangu, ambaye amewalea watoto kadhaa kwenye familia pia alisema ukuaji wake haukuwa wa asili. Hapo ndipo tulipompeleka kwa daktari.’

Imetafsiriwa kutoka  news.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo