Breaking News Makete: Shule ya Sekondari Kitulo imefungwa (Audio)

Katika hali isiyotarajiwa shule ya sekondari Kitulo kata ya Kitulo wilayani Makete mkoani Njombe imefungwa kabla ya muda wa kuanza likizo kufika kutokana na upungufu wa chakula cha kuwapa wanafunzi

Taarifa zinasema shule hiyo imefungwa Jumatano iliyopita Mei 25 mwaka huu huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ni upungufu wa chakula cha wanafunzi

Awali Kabla ya kufika shuleni hapo mwandishi wetu amefika kwenye uongozi wa kijiji na Kata kujua sababu za shule hiyo kufungwa ambapo Afisa mtendaji wa Kijiji cha Ujuni, pamoja na mwenyekiti wake wamesema hawana taarifa za kufungwa shule hiyo na kwa mara ya kwanza ndiyo wanazisikia kwa mwandishi wetu

Diwani wa Kata ya Kitulo Mh Asifiwe Mahenge amekiri kuwa na taarifa za kufungwa shule hiyo kutokana na upungufu wa chakula jambo ambalo amesema limetokana na viongozi wa kata kutoshirikishwa na uongozi wa shule hiyo kuhusu tatizo la upungufu wa Chakula

Amesema wao kama wangeshirikishwa wangehakikisha wanapigana kwa hali na mali hata kwa uwatafuta wadau wachangie upungufu wa chakula kinachohitajika wakati wakitafuta namna ya kukirudisha baada ya wazazi kuchangia

Diwani Mahenge amesema kwa sasa wanasubiri kikao hicho cha tarehe 03 Juni mwaka huu kwa kuwa anaimani majadiliano hayo yataleta muafaka wa suala hilo

Mwandishi wetu amefunga safari hadi shuleni hapo na kukutana na makamu mkuu wa shule Mwl Degdus Ezekiel Mwatujelele ambaye amesema ni kweli shule hiyo imefungwa kwa muda hadi Juni 03 ambapo wanafunzi wametakiwa kwenda na wazazi wao, na sababu ya kufungwa shule hiyo ni upungufu wa chakula cha wanafunzi

Amesema baada ya uongozi wa shule kupata taarifa za upungufu wa chakula ikatangazwa na mkuu wa shule kuwa wanafunzi wote warudi nyumbani mpaka Juni 03 Mwaka huu kila mmoja aje na mzazi wake waweze kuwa na mjadala wa pamoja kwa kuwa upungufu huo wa chakula umesababishwa na baadhi ya wazazi kutochagia chakula kama walivyokubaliana

Kwa mujibu wa makamu mkuu huyo wa shule ni kwamba shule hiyo ni ya kutwa isipokuwa wanafunzi wa kike wanalala kwenye daharia za shule (hostel)

Afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Mwl. Jacob Meena amesema hana uhakika sana kama shule hiyo imefungwa kwa sababu ya upungufu wa chakula  kwa kuwa shule hiyo ni ya kutwa lakini anachokifahamu ni kwamba kwa kuwa wanafunzi wamemaliza mitihani na kwa sasa kuna shughuli nyingine zinazoendelea kufanyika mpaka Juni 03 watakapopewa matokeo yao

Amesema kwa sasa anachokifahamu walimu kwa sasa wapo kwenye heka heka za kusahihisha mitihani na kupanga matokeo kwa kuwa agizo lililotolewa ni kwamba wanafunzi wapewe matokeo yao wakati shule inafungwa na si inapofunguliwa

 Muonekano wake baada ya kufungwa



Sikiliza sauti Diwani, Afisa elimu na Makamu mkuu wa shule bonyeza play hapo chini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo