M toto wa marehemu Anathe, Allan Kimario (aliyelala).
Majonzi na huzuni vimetawala
kwenye tukio la kuagwa kwa mwili wa mdogo wa Bilionea Erasto Msuya
aliyeuawa kwa risasi mwaka 2013, Anathe Simon Msuya ambaye yeye
aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar, Mei 25
mwaka huu.
Mamia ya waliofika katika Kanisa la KKKT
Usharika wa Mashariki, Salasala jijini Dar wakiwemo wafanyakazi wenzake
wa Wizara ya Fedha alikokuwa akifanya kazi marehemu, walishindwa
kujizuia kuangua vilio walipokuwa wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na
mwili huo kutoa heshima zao za mwisho.
Mtoto wa Anathe aliyetajwa kwa jina la
Alan Kimario (4) alionekana akilazimishwa kwenda kuuaga mwili wa mama
yake kwani alikuwa akitaka aachwe aendelee na michezo yake kutokana na
ukweli kwamba, alikuwa hajui hata kinachoendelea.
Mwili wa marehemu Anathe umesafirishwa
kwenda Mererani jijini Arusha kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa
kufanyika kesho (Jumanne).
Mungu ailaze roho ya marehemu Anathe mahali pema peponi. Amin!
PICHA NA DENIS MTIMA/GPL