Wizi kushamiri Tandala, Wananchi watoka na maamuzi Magumu

Wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wameazimia kufuatwa kwa sheria za kijiji hicho ambazo wanadhani ni kichochezi cha vitendo viovu katika kijiji hicho

Moja ya mambo waliyoyaamua yafuatwe ni pamoja na kuzingatia muda wa kufunga na kufungua sehemu za kuuzia vileo yaani kwenye mabaa na vilabu vya pombe za kienyeji

Wananchi hao wameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji hicho ambapo wamesema kwa hivi sasa kumekuwa na vitendo viovu vilivyozuka katika kijiji hicho ukiwemo wizi wa pikipiki pamoja wizi katika maduka

"Sasa hivi unakuta sehemu wanazouzia pombe hakuna muda wa kufunga wala kufungua, muda wowote mtu akijisikia anafungua, sasa wakati mwingine unakuta wahalifu ndio wanajificha huko, sasa hivi hapa kijijini kuna wageni wengi tu hata hakuna mtu anayewauliza kuwa wametoka wapi wala nini, kwa kweli mwenyekiti kuna haja ya kufuatilia sana utekelezaji wa sheria zetu ndogondogo za kijiji" amesema Mwananchi mmoja ambaye hakutaja jina lake

Akiwauliza wananchi katika kikao hicho Mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Bw. Andowise Memba amesema "Je wananchi mnaridhia kuwa haya mapendekezo yenu yote yatekelezwe na mamlaka zinazohusika mara baada ya kikao hiki?" ndipo wananchi hao walipojibu kuwa wamekubali maazimio hayo yatekelezwe
Diwani wa kata hiyo Mh Egnatio Mtawa (pichani kushoto) ameahidi kufuatilia maazimio yote waliyoyaamua wananchi katika kikao hicho na kuyakumbusha kuwa ni kuzingatia muda wa kufunga na kufungua sehemu za kuuzia vileo, uwepo wa vikundi vya sungusungu usiku, vibali vya kupiga disko usiku kuwa mwisho ni saa sita na nusu

"Mtendaji ninakuagiza hili halina mjadala maana limeamuliwa na wananchi katika mkutano mkuu, kwetu sisi ni utekelezaji tuu, na kazi hii ianze leo muda wa kufunga na kufungua vilabu na baa uzingatiwe na tukianza kutekeleza hili wananchi tunaomba msitulaumu, na pia kabla ya maazimio haya nilishaagiza kwa afisa biashara wa wilaya kuwa vibali vyote vya kupiga mziki makete mwisho saa sita na nusu usiku na tutasimamia iwe hivyo" amesema Mtawa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo