Watumishi hao waliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini nchini walitakiwa kutoka nje ili kuwapisha wajumbe hao kujadili baadhi ya mambo waliyodai kuwa ni muhimu kwa taifa ambayo yaliibuka ndani ya kikao hicho kwa madai ya kutoridhika na majibu ya ujumbe huo wa TANESCO.
Baada ya wajumbe kujadiliana walikuja na maamuzi ya kuitaka TANESCO kuanza uchunguzi wa kina kwa uhalali wa wafanyakazi wao kwa kuanzia na uongozi ikiwabidi wajiuzulu nyadhifa zao walizonazo kwa sasa kwakuwa hawana uwezo utakaowapa uhalali wa wao kuendelea na kazi kwa serikali hii ya awamu ya tano na kumuomba Rais wa Tanzania afanye mabadiliko ndani ya TANESCO.
Kwa upande wao viongozi wa TANESCO pamoja na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Prof. Justus Ntalikwa na Mkurugenzi Eng. Felsechmi Mramba wamesema kuwa tatizo linaloikumba kwa sasa TANESCO ni mikataba mibovu iliyoingiwa kipindi cha nyuma.