Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijuakali (Pichani) amekamatwa na jeshi la Polisi kwa zuio la kutosogelea eneo la uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kilombero uchaguzi ambao unaendelea hivi sasa.
Tukio hilo limetokea mapema masaa kadhaa yaliyopita kutoka Kilombero, Mkoani Morogoro ambapo uchaguzi huo unafanyika. Mbali na kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Kilombero ambaye alitaka kuingia kama Mjumbe halali na mpiga kura, taarifa zinaeleza kuwa, pia dereva wa Mbunge huyo pamoja na dereva wa Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Morogoro, Devotha Minja wote wamekamatwa. Hata hivyo habari zinaeleza kuwa, licha ya uchaguzi kuendelea baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari wamezuiwa kuingia kuripoti habari hizo huku waandishi wa vyombo vya Serikali na chama cha Mapinduzi CCM, ambao waliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ndiyo pekee walioruhusiwa kuingia katika uchaguzi huo.