Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.
Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Justus Kamugisha amesema hati ya kukamatwa kwake imetoka ofisi ya Bunge na kwamba Mbunge huyo anashikiliwa kama mtuhumiwa ambaye anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.
Wabunge hawa pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA Wako jijini Mwanza kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest

#Habari:Mbunge wa jimbo la Bunda Ester Bulaya amekamatwa na Polisi Mwanza,haijafahamika nini sababu za kukamatwa na tayari viongozi wakuu wa CHADEMA wameelekea kituoni hapo kujua sababu.
Posted by ITV Tanzania on Friday, March 11, 2016