Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Francis Namaumbo akifafanua jambo
Watendaji wa kata na vijiji wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa
kutenda majukumu yao vizuri kama sheria zinavyowataka ili kuepusha migogoro na
matatizo yanayoweza kutokea pindi wanapokiuka sheria hizo
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutoa risiti za malipo wanayoyafanya
katika kata ama vijiji vyao pamoja na kusoma mapato na matumizi kwa wananchi
wao
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete
Bw. Francis Namaumbo katika kikao maalum kilichowakutanisha kwa pamoja
watendaji wote wa vijiji na kata wilayani Makete kwa lengo la kukumbushana
mambo mbalimbali wanayotakiwa kuzingatia katika kutekeleza majukumu yao
Afisa utumishi wa wilaya ya Makete Bw. Nicodemus Tindwa
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio
Mtawa amesema pamoja na watendaji hao kutakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata
sheria na taratibu za kazi, lakini atasimamia haki zao kama wafanyakazi pamoja
na kusimamia mazingira mazuri ya watendaji hao kutekeleza majukumu yao vizuri
bila vikwazo mbalimbali
Aidha katika kikao hicho watendaji hao wamepata nafasi ya kuzungumzia
changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi ikiwemo na wao kujengewa
nyumba za kuishi kama zinavyojengwa kwa watumishi wengine katika maeneo yao