Imani za Kishirikina zakutana na Kipindupindu Kyela, Matokeo yake yako hapa

NA KENNETH NGELESI,MBEYA

IMANI za kishirikina miongoni mwa jamii ya wananchi katika wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, zinatajwa kuwa ni moja ya sasababu zinazo kwamisha juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa tishio kwa maisha ya wananchi  kutokana na kutokea mara kwa mara Wilayani humo.

Hayo yamebanishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dk Theo Ntara mara baada ya kumalizika kwa kikao chake na Mafisa watendaji wa kata kutoka kata zote za Wilaya hiyo ambo kilikuwa kwa ajili ya kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa huo.

Akizungumza na edwinmoshi.blogspot.com Mjini Kyela  DK Ntara alisema kuwa imani za kishirikina zinachangia kwa kiasi kukubwa kukwamisha juhudi za Serikali za kupambana na ugongwa huo ambao unatokana kikidhiri uchafu, kwani watu wengi wano ugua wamekuwa wakiamini wamerogwa.

Alisema kuwa jamii ya Watu Kyela hawana utamaduni kuchimba vyoo na badala yake  wamekuwa wakijisaidia kwenye Mikokoa, Mito na Ziwa Nyasa wakati huo huo wanatumia maji hayo kupikia na kunywa ndiyo maana imekuwa ngumu sana kupamba na ugonjwa huu.

‘Hawa ndugu zangu hawana utamaduni wa kujimba Vyoo kwani kila wanapo hitaji kujisadia haja zote kubwa na ndogo wamekuwa wakienda kwenye mashamba ya Migomba,Mikokoa , Mito na ziwa Nyasa na wakati huo huo maji hayo yanatumika kwa matumizi ya nyumbani na ndiyo maana ugonjwa umekuwa ukitokea mara kwa mara katika Wilaya yetu na wote tunajua ugonjwa sehemu unatokana na kula kinyesi’ alisema Ntara

Dt Ntara alisema kuwa wameamua kukutana na watendaji hao ili kuwapa mikakati ya kupambana na ugonjwa huo huku akiigaiza wamiliki wote wa migahawa,Vilabu vya pombe za kienyeji kusimamisha mara moja huduma hiyo mpaka watakapo jiridhisha ugonjwa huo kutokuwepo tena Wilayani humo.

Alisema kuwa jukumu la watendaji hao ni kuhakikisha wanaenda kusimamia kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo na kwamba mtendaji yoyete ambaye ugonjwa huo utaonekana kuibuka katika eneo lake atapaswa kutolea maelezo huku akiwagiza kuwachukua hatua dhidi ya wanasiasa ambao wataonekana kuwa kikwazo kwao wakati wa utekelezaji wa maagizo.

 ‘Nafahamu kikwazo kingine ni kutoka kwa  wanasiasa hasa wenyeviti wa Vijiji na Madiwani pindi watakapo anza kutekeza maagizo hasa hili kufunga vibabu migahawa na kuzia huduma ya chakula misibani wanaweza kuanza kuleta vikwaza nimewambia watendaji wakiona wanakwamishwa wasisite kuwachukulia hataua hata ndani na pia tuleteeni taarifa kwani huu muda siyo wa siasa wakati watu wanaumia” alisema Ntara.

Akifafanua zaidi suala la chakula Dt Ntara alisema kuwa endapo kuna msiba umetokea watu wanatakiwa kuzika na kutawanyika kusiwepo na huduma yeyote na chakula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Clemence Kasongo alisema kuwa katika kipindi cha Februal /Machi  hakuna aliyefariki dunia lakini watu wamekuwa wakiuguwa wamekuwa wakitibia na kurudi kwao ambapo mpaka sasa kuna wagonjwa watatu.

Aidha alibainisha kata ambazo zimekuwa zikikumbwa na ugonjwa huo huo mara kwa mara kuwa Ipande,Ipinda,Makwale,Matema,Ndobo,na Lusungu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo