Ibada Ya Kuuaga Mwili Wa Marehemu Sarah Dumba Imeongozwa Na Askofu Wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheli Tanzania Dayosisi Ya Kusini Issaya Japhet Mengele Na Kuhudhuriwa Na Viongozi Wa Vyama Vya Siasa,Dini Na Serikali Akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Filemon Luhanjo, Barozi Mstaafu Godone Ngilangwa Na Askofu Wa Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Alfred Maluma.
Askofu Wa Kanisa La KKKT Dayosisi Ya Kusini Issaya Japhet Mengele Akiongoza Ibada Hiyo Amesema Watumishi Mbalimbali Wa Serikali Wanatakiwa Kurudisha Heshima Kwa Mungu Kama Alivyokuwa Akilitumikia Kanisa Hilo Marehemu Sarah Dumba Kwani Binadamu Hajui Siku Wala Saa Yakuchukuliwa Na Mungu.
Aidha Askofu Mengele Amesema Marehemu Sarah Dumba Ameonesha Mfano Wa Kufanya Kazi Kwa Watumishi Wengine Wa Serikali Na Wasiyo Wa Serikali Na Kwamba Mungu Hana Chama Na Wala Cheo Bali Binadamu Wote Sawa Na Njia Ya Kuelekea Mbinguni Ni Moja Huku Akisema Marehemu Alionesha Uadilifu Mkubwa Kanisani.
Akizungumza Mara Baada Ya Kuuaga Mwili Wa Marehemu Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Filemon Luhanjo Amesema Waandishi Wa Habari Wanatakiwa Kuiga Mfano Wa Marehemu Huyo Ambaye Ametunukia Tuzo Mbalimbali Kutokana Na Uandishi Wake Huku Akisema Amemfahamu Zaidi Wakati Marehemu Akihamasisha Wakulima Kulima Zao La Chai Ili Kuondoa Umasikini Miongoni Mwao.
Kwa Upande Wake Katibu Wa CCM Wilaya Ya Njombe Sadakat Kimatt Amesema Enzi Ya Uhai Wake Sarah Dumba Alikijenga Chama Cha Mapinduzi Katika Nyanja Mbalimbali Kanzia Kwenye Kamati Ya Siasa Huku Akisema Atakumbukwa Kwa Kutumikia Chama Vizuri Kwa Kutekeleza Ilani Ya Chama Na Kusimamia Vizuri Halmashauri Tatu Na Kuhimiza Maendeleo.
Mwili Wa Marehemu Sarah Dumba Ambaye Alikuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Unatarajia Kuzikwa Kigamboni Jijini Dar Es Salaamu.
KUSHOTO NI ASKOFU ISSAYA JAPHET MENGELE NA KULIA NI MAKAMU ASKOFU DKT GEOGE FIHAVANGU
ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA KUSINI ISSAYA JAPHET MENGELE AMEONGOZA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SARAH DUMBA KATIKA KANISA HILO
MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AKITOKA KUSOMA HISTORIA YA MAREHEMU
HII NDIYO PICHA YA MAREHEMU SARAH DUMBA
WAUMINI MBALIMBALI WA KIWA KANISANI HAPO KWAAJILI YA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA
KATIBU MKUU KIONGOZI MSTAAFU FILEMON LUHANJO AKIWA NA VIONGOZI WA BENK YA CRDB AKIWEMO MENEJA WA BENK HIYO WAKIWA KWENYE MSIBA YA SARAH DUMBA
HAPA MWILI UKIWASILI KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA ILEMBULA UKIFIKA NYUMBANI KWAKE -IKULU NDOGO
Chanzo:Michael Ngilangwa