Agizo la Rais Magufuli tayari limefika Makete...Mkurugenzi wa Halmashauri aongelea utekelezaji wake

Ikiwa zimesalia siku 12 katika siku 15 alizoagiza Rais John Magufuli kuwa wakuu wa mikoa washughulikie halmashauri ziwaondoe watumishi hewa katika malipo ya mishahara ya watumishi wa serikali, Wilaya ya Makete imeeleza ilipofikia

Akizungumza nasi Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Francis Namaumbo amesema agizo hilo la rais wamelipokea na halina mjadala katika utekelezaji wake kwani wameshaanza kulitekeleza

Amesema wamekuwa na utaratibu wa kupitia orodha ya watumishi mara kwa mara kujiridhisha kuwa hakuna watumishi hewa na wanaendelea kufanya hivyo mpaka sasa na kuongeza kuwa endapo watabaini kuna mkuu wa idara au mtumishi ambaye anashiriki mchezo huo mchafu pia atachukuliwa hatua mara moja

"Agizo la Rais tumelipokea na halina mjadala katika kulitekeleza, tutalitekeleza kwa kuhakikisha tunawaondoa watumishi hewa katika halmashauri yetu kama watakuwepo ili kuepuka dosari katika agizo hilo la Mheshimiwa Rais" amesema Namaumbo

Machi 15 Rais Magufuli mara baada ya Kuwaapisha wakuu wa mikoa Ikulu jijini Dar Es Salaam amewaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha ndani ya siku 15 wanawaondoa watumishi wote hewa katika halmashauri zao, na katika mshahara wa mwezi huu wa tatu endapo kutakuwa na halmashauri itakayopeleka orodha ya watumishi hewa katika kulipwa mishahara, mkurugenzi huyo atavuliwa madaraka papo hapo na kufikishwa mahakamani na Mkuu wa mkoa husika itadhihirisha kuwa hatoshi katika nafasi yake hiyo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo