![]() |
YULE omba omba maarufu wa mjini Iringa, Mohamed Chengulla anayetumia kisu kuwatisha watu anaotaka wamsaidie fedha amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa baada ya msako mkali kufanywa dhidi yake. |
Kijana huyo alikamatwa leo leo majira ya saa 5 asubuhi katika eneo la Posta mjini Iringa baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi, hasa wanawake ambao wamedai kufukuzwa mara kwa mara na kijana huyo akiwa na kisu chake mkononi baada ya kunyimwa pesa anazotaka kusaidiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba pamoja na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo ametaka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo pindi wanapoona au kukutana na matukio yanayohatarisha usalama wa mali na maisha yao.