Wanafunzi hawa wa Makete waomba MUNGU wazazi wao wafe wabaki yatima..!!!!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wanafunzi wanaosoma katika shule ambayo jina lake linahifadhiwa iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe wanaomba wazazi wao wote wafe na wao wabaki yatima ili walelewe maisha ya ufadhili ambayo wamesema ni mazuri kuliko wanayoishi sasa

Hayo yamesema na mzazi mmoja wakati akizungumza kwenye kikao cha wazazi kilichofanyika katika shule ya Msingi Ludihani kata ya Iwawa mji mdogo wa Iwawa Makete mjini, ambapo amesema kutokana na wazazi kusahau kuwahudumia watoto wao kwa kuwapa mahitaji muhimu ya shule hasa mavazi, jambo hilo limepelekea watoto hao kuombea wazazi wao wafariki dunia kwa kuwa watoto yatima hupatiwa mavazi na vifaa vingine vya shule kutoka kwa wafadhili mbalimbali

"Kuna watoto yatima hapa wanafadhiliwa na wahisani wanapatiwa mahitaji yao yote kwa wakati, wazazi wenzangu tunaendekeza starehe kwa wingi tunasahau kuwahudumia watoto sasa unategemea watoto wako awahudumie nani?, na ndio maana nilipita kwenye shule X nikakuta watoto wanasema yatima wanahudumiwa kila kitu ila sisi wenye wazazi hatuhudumiwi ipasavyo, ni heri na wazazi wetu wafe ili na sisi tuhudumiwe vizuri kwa kuwa tutakuwa yatima" amesema mzazi huyo ambaye hakujitambulisha jina
Mwalimu mkuu shule ya msingi Ludihani

Awali katika kikao hicho Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ludihani Onesmo Chang'a amewasisitiza wazazi hao kuwapatia sare mpya za shule kwa kuwa baadhi ya wanafunzi wanatia huruma kwa kuvaa sare zilizochakaa ilihali wazazi wao wanauwezo wa kuwahudumia

Mwalimu Chang'a amesema huu sio muda wa kufanya masihara na badala yake wazazi wajenge mazoea ya kuwalea watoto wao kwa kuwa ni wajibu wao na pia baadhi ya wanafunzi katika shule yake wamekuwa wakiathirika kisaikolojia na kushindwa kuzingatia masomo pindi wanapowaona wenzao wamevaa sare mpya wazizopatiwa na wazazi wao

Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani Makete kwenda shuleni wakiwa wamevaa sare zilizochakaa jambo ambalo limekuwa kero kwa wanafunzi hao pamoja na walimu na jamii inayopenda maendeleo ya watoto, hivyo wazazi kutakiwa kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwahudumia watoto hao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo