Mashoga wafungwa maisha kwa kumuua mteja wao

sentence-538x458
Mashoga hao wakiwa mikononi mwa polisi, picha ndogo(kushoto) ni mteja wao aliyedaiwa kuuawa.

JAJI wa mahakama moja huko Manhatan, jijini New York, Marekani, amewahukumu mashoga wawili wa kiume kifungo cha maisha kwa kumuua mteja wao wa siku nyingi katika makazi yake eneo la Chelsea.

Mashoga hao (pichani) Edwin Faulkner (kushoto) mwenye umri wa miaka 33 na Juan Carlos Martinez-Herrera ( 35) watayamalizia maisha yao gerezani.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Bonnie Wittner katika mahakama hiyo jana.  Watu hao walimkaba kwa kumziba pumzi na kumwibia mteja wao huyo, John Laubach (57) Machi 2, 2012.

“Alikuwa mteja wangu, tulikuwa tunakwenda kwake kila mara ambako alikuwa ananilipa kwa kufanya naye ngono,” alikiri Martinez-Herrera katika mahakama hiyo.

Wawili hao walimwibia Laubach vito mbalimbali na vitu vingine vya thamani kabla ya kutorokea Jimbo la Miami.
Martinez-Herrera, ambaye alikuwa amevaa nguo za kiume wakati alipokamatwa, alitokea mahakamani akiwa na nywele ndefu na akizungumza kwa sauti ya kike.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo