Mafuriko yavamia Mlimani City

MVUA kubwa iliyonyesha Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana   imesababisha maji kuingia na kujaa ndani ya jengo maarufu la maduka ya biashara la Mlimani City lililopo pembezoni mwa barabara ya Sam Nujoma.
blog hii ilifika eneo hilo na kushuhudia maji yakiwa yametuama na kujaa katika maduka mbalimbali likiwamo duka kubwa la Nakumat, Duka la Sumsung na benki ya KCB Tawi la Mlimani City huku wafanyakazi wa jengo hilo wakihangaika kuyatoa nje kwa kuyachota.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB, alisema mvua hiyo ilisabababisha maji kujaa katika eneo ambalo ujenzi unaendelea, lililopo pembezoni mwa jengo hilo na baadaye maji hayo yaliingilia mlango wa nyuma uliopo karibu na benki hiyo.
Alisema maji hayo yamesababisha athari kubwa kwa benki hiyo ikiwamo kuungua  baadhi ya vifaa vya umeme na kuchelewesha muda wa kufungua benki.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo