Zahanati ya kijiji cha Ndulamo wilaya ya Makete ambayo imeanza kutoa huduma
Mwenyekiti wa kitongoji cha Ngiu wilayani Makete mkoani Njombe akizungumza na mwandishi wetu
Mmmoja wa mwanamke aliyempeleka mwanaye kupata huduma kwenye zahanati hiyo
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ndulamo Majuto Mbwilo akizungumza na mwandishi wetu kijijini hapo
Mganga mfawidhi wa kituo hicho akizungumza na mwandishi wetu
Wananchi wa kijiji cha Ndulamo Kata ya Iwawa mji mdogo wa Makete mkoani Njombe wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya baada ya zahanati ya kijiji hicho kuanza kufanya kazi
Wakizungumza na Eddy blog wananchi hao wamesema awali walikuwa wakifuata huduma hiyo hospitali ya wilaya ya Makete ambayo ipo umbali na hivyo kufuatia huduma hizo kuanza kutolewa wanaona neema ya kujitoa kwa hali na mali kushirikiana na serikali
habari/Picha na Edwin Moshi