Kesi ya msingi ya kupinga Ubomoaji wa nyumba zilizopo kwenye mabonde ya wakazi wa jimbo la Kinondoni iliyofunguliwa na Mbunge wa jimbo hilo, Maulid Mtulya (CUF) ambayo inataka wananchi hao mbali na kubomolewa wapewe maeneo mbadala na yenye usalama, iliyofunguliwa Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi, jijini Dar es Salaam, imesogezwa mbele hadi hapo 25 Januari itakapotolewa hukumu.
Akizungumza na wananchi pamoja na wanahabari, Mbunge huyo, amebainisha kuwa, baada ya leo Januari 14, kufika mahakamani hapo na pande zote kuendelea na mashahuriano, ikiwemo Mbunge huyo la kuweka zuio la muda la kutobomolewa kwa nyumba zote za Mabondeni ndani ya jimbo la Kinondoni, Hata hivyo waendesha kesi wamesogeza mbele hadi hapo 25 Januari, majira ya saa nane mchana itakapotolewa mahamuzi kamili.
Awali nje ya mahakama hiyo iliyopo katikak jengo la Shirika la Nyumba eneo la Posta, ilijaa na umati mkubwa wa wananchi wa mabondeni wakiwemo wale waliobomolewa nyumba zao pamoja na waliowekewa alama nyekundu ya X, wakisubiria hukumu hiyo.
Hata hivyo baada ya kuharishwa kwa kesi hiyo, wananchi hao walitoa dukuduku lao kwa Serikali kuchukua hatua ya haraka kumaliza hilikujua hatima yao.
