Taasisi ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na umwagaji wa damu.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Musoma, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo mzee Joseph Butiku, amesema amekerwa na tabia ya ZEC kusitisha uchaguzi na kushindwa kuwatangazia wananchi kiongozi wao waliomchagua, huku ikishindwa kuheshimu matakwa ya wananchi waliopiga kura katika visiwa vya Zanzibar.
Aidha mzee Butiku amewataka wananchi wa Zanzibar kutokubali tena kurudia upigaji wa kura hadi hapo yatakapotolewa maelezo ya kuridhisha na wahusika waliosababisha uchaguzi huo kufutwa pia waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria
Kwa sababu hiyo amewataka viongozi kuheshimu sheria na katiba ya nchi na kwamba chama ambacho kinadhani kimeshindwa katika uchaguzi huo kikubali matokeo badala ya kuifanya zanzibar ni mali ya chama fulani pekeee.