Umeipata hii ya mkuu wa mkoa wa Dodoma na Pombe? Hebu isome

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi. Amri hiyo ameitoa jana katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari.

Gallawa alisema kwamba amechukua uamuzi huo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 61, Ibara ndogo ya 4.
 
Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na wafanyabiashara wa mkoa huo kuuza au kunywa pombe kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kusimamia utekelezaji wa amri hiyo na kuongeza kuwa yoyote atakayekiuka amri hiyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo