Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma na wananchi kwa ujumla kwamba imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Awali majira ya saa 6: 00 mchana leo Novemba 6, mwaka huu Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha ya Rais, ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa gharama ya Shilingi Elfu Kumi na Tano tu (15,000/=).
Aidha, Serikali imesema kwamba itazitangazia ofisi hizo na umma wa Watanzania kuhusu kuanza tena kwa matumizi ya picha hiyo hapo baadae.
Imetolewa na
IDARA YA HABARI.
Novemba 6, mwaka 2015