Mke wa Lowassa Akataa Ubunge Aliopewa na CHADEMA

Mke wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, Regina Lowassa, ameikataa nafasi ya ubunge wa viti maalum aliyopewa na kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani.

Kwa mujibu taarifa wa kutoka familia ya Lowassa iliyotufikia, Regina anaichukulia kwa heshima kubwa nafasi hiyo, lakini anaamini ataweza kushughulikia matatizo ya akina mama na watoto akiwa nje ya bunge.

"Naishukuru kamati Kuu ya chama changu kwa heshima hii kubwa waliyonipa na ninaithamini sana, lakini naamini nitaendeleza mapambano ya kuwaletea akina mama mabadiliko kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge," amesisitiza mke huyo wa waziri mkuu wa zamani katika taarifa hiyo.

Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kumpa Regina nafasi ubunge viti maalum kutokana na mchango mkubwa aliyoutoa wakati wa kampeni ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia upatikanaji wa majimbo mengi tofauti na uchaguzi wa mwaka 2010.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo