Tume ya taifa ya uchaguzi imeendelea na msimamo wa kutoruhusu wananchi kubaki katika vituo vya kupigakura baada ya zoezi la kupiga kura na kusisitiza itatambua ushindi wa mgombea katika ngazi yeyote ambao umejengeka katika misingi ya sheria, kanuni, taratibu na kwa kuzingatia kura halali.
Akizungumza katika mkutano wa mwisho wa tume na viongozi wa vyama vya siasa baada ya kuibuka kwa hoja ya mazingira ya kuwepo kwa bao la mkono, mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi, jaji mstaafu Damian Lubuva amesema tume haina msamiati wa bao la mkono na inapenda kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na amani na ili kuhakikisha viashiria vya vurugu vinatokweka.
Katika mkutano huo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wametaka kuwepo kwa mfumo wa kujumlisha matokeo unaenda sambamba na wa tume ya taifa ya uchaguzi kwa kila taasisi ikiwemo vyombo vya habari kwa lengo la kudumisha uwazi na kuepuka uchakachuaji na kudumisha amani na utulivu.
Aidha kuhusu wapigakura kulinda kura katika vituo, viongozi wa vyama wamekuwa na mitazamo tofauti huku baadhi wakionyesha kuwa na imani na tume ya taifa ya uchaguzi toka kuanza mchakato wa uchaguzi nchni,huku wengine wakiendelea kusisitiza hafu ya wanachi kutaka kulinda kura yanatokana na uzoefu katika chaguzi zilizopita na kusababisha kutokuwa na imani na tume ya taifa ya uchaguzi.