Jamaa atoa kituko cha mwaka mahakamani

Kiongozi wa kidini ameitamausha mahakama moja nchini India alipoiambia kuwa hatoweza kufika mbele yake hadi baada ya miezi 8 kwani hawezi kupanda gari..
Kisa ?
Kiongozi huyo wa dhehebu la Jain alisema kuwa hawezi kupanda gari kwani ni inakiuka imani yake kali na kanuni za dini yake.
Bwana Acharya Kirti Yashurishwarji Maharaj anasema kuwa kwa sasa yuko katika jimbo la Kolkata,zaidi ya kilomita 2,000 kutoka mahakama hiyo iliyoko katika mji wa Ahmedabad Magharibi mwa India.
Yashurishwarji Maharaj anasema iliaupokee uongozi wake wa kidini ilimbidi kuukata ulimwengu na malimwengu kwa hivyo hawezi kushiriki mambo ya ulimwengu ikiwemo magari.
Mahakama hiyo hata hivyo imekatalia mbali ombi lake la kutaka kesi hiyo iahirishwe.
Bwana Acharya Kirti Yashurishwarji Maharaj anakabiliwa na tuhuma za kughushi vyeti rasmi vya serikali vilivyomruhusu kuwashawishi watoto wa kihindi kujiunga na itikadi hiyo ya Jain.
Ushawishi wa watoto kujiunga na madhehebu yeyote yanakwenda kinyume cha sheria za kuwalinda watoto nchini India.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo