Hii hapa idadi ya waliojiandikisha kushiriki kupiga kura Uchaguzi 2015

leo Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Kombwey ametoa takwimu au idadi ya watanzania waliojiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye Uchaguzi mkuu 2015.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo Octoba 12, 2015 alisema…’Leo tume ya Uchaguzi ilikuwa imekutana na vyama vya kisiasa kuwapa taarfia kuhusu maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 25 kwasababu zilikuwa zimebaki siku 12 au 11 sasa miongoni mwa taarifa za msingi ambazo walikuwa wazipate kwanza kuhusu shughuli za mchakato wa daftari la upigaji kura limeshatoka na tayari yameshapelekwa mikoani’ –Kailima Kombey
Tume ya taifa ya uchaguzi ilitoa ilitoa taarifa ya awali takwimu ya watu walioandikishwa ni idadi ya watu milioni 23,782,558 hiyo ndio taarifa ya kwanza tulizozitoa  za jumla za wapiga kura waliojiandikisha na takwimu zilizotoka kwenye vituo vya kupigia kura tume ikabaini watu 181,452 walikuwa wamejiandikisha zaidi ya mara mbili wameshatolewa kwa hiyo takwimu zao zimeondolewa’ – Kailima Kombey
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo