News Alert: Kuhusu Vipindi vinavyorushwa "live" wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kuwa kuanzia leo tarehe 10 Septemba 2015, na katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge, urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama wawakilishi hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja (Live Programmes) vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji.

Utaratibu huu unazingatia Kanuni Za Huduma Za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji Wa Uchaguzi Wa Vyama Vya Siasa), 2015, Kanuni ya 4 (f), (h), (i),  5(b), (d), (e) and (f).

Hatua hii inachukuliwa na Mamlaka ili kuweka utaratibu mzuri wa kufanya kampeni za uchaguzi ziwe za amani na utulivu.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kituo cha utangazaji kitakacho kwenda kinyume na utaratibu huu..

IMETOLEWA NA:
Mkurugenzi Mkuu
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo